Maafisa wa afya ya jamii katika kaunti ya Nyamira wamelalamikia changamoto nyingi wanazopitia kwa kutekeleza kazi yao.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi hao, msimamizi mkuu wa afya ya jamii Charles Omari Mogaka alisema kwamba maafisa hao hawana vifaa vya kutosha vya kufanya kazi.

Mogaka pia amedokeza kuwa ni wachache kiidadi hali ambayo huwapeleka kufanya kazi nyingi zaidi katika sehemu mbalimbali.

Alisema kwamba changamoto kama vile ukosefu wa nauli ni miongoni mwa sababu nyingine ambazo zinafanya kazi kuwa ngumu.

Mogaka alisema kwamba atawasilisha wito wao kwa serikali ya kaunti ili kuona kama shida zao zitapata kusuluhishwa.

Wametoa mwito kwa serikali ya kaunti hiyo kuingilia kati na kuwasaidia ili waweze kutekeleza wajibu wao inavyostahili.

Madaktari na wauguzi nchini wamekuwa wakigoma wakilalamikia changamoto kama vile mishahara duni na pia mazingira magumu ya kazi.

Sekta ya afya nchini imeathirika pakubwa na shida mingi zimewapelekea madaktari wengi kuhamia taaluma zingine na hata wengine kuhamia nchi zingine.