Maafisa wa polisi wameanza msako wa nyumba kwa nyumba katika eneo la Kisauni kutafuta silaha hatari zikiwemo bunduki na mapanga, zinazoaminika kumilikiwa na vijana wa kundi la uhalifu la Wakali Kwanza.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akithibitisha kuwepo kwa msako huo kwenye mahojiano kupitia njia ya simu siku ya Jumamosi, afisa mkuu wa polisi katika eneo la Kisauni, Richard Ngatia, alisema kuwa waliamua kutekeleza msako huo baada ya kupata taarifa kuwa kuna bunduki zilizokuwa zikitumiwa na vijana hao katika kutekeleza uhalifu.

“Msako huo utaendelea hadi wakati ambapo tutaridhika kama Idara ya Usalama kuwa hakuna silaha hatari katika eneo la Kisauni,” alisema Ngatia.

Kumekuwa na hali ya sitofahamu katika wiki iliyopita baada ya vijana hao kukabiliana vikali na maafisa wa polisi huku mmoja wao akichomwa na wakaazi wa eneo hilo.