Polisi waliojifanya walevi walimtia mbaroni mgema pombe harama mmoja, huku pombe mitungi kumi ikimwagwa na maafisa hao katika kata ya Nyamusi.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Maafisa hao wamekua katika msako mkali, na wakamwaga pombe hiyo iliyokuwa imefichwa shambani. 

"Tumekuwa tukijifanya walevi tunapokuja hapa na kufahamu siri zote kuhusiana muuzaji huyu wa pombe. Leo tumemtia mbaroni bila yeye kutarajia na tukamwaga pombe mitungi kumi ambayo alikuwa amezika mchangani," alisema afisa mmoja.

Chifu wa eneo hilo Elijah Gesora amewaonya wote wanaondesha biashara hizo haramu kuwa warekebishe kabla ya kuchukuliwa hatua za kiserikali.

"Nataka kuwambia kuwa hili ni funzo kwa wale wenye tabia kama hii ya kuuza pombe kijijini, na hao wote warekebishe kabla ya serikali kutua katika makazi yao," alisema chifu huyo.