Maafisa wa serikali wa kaunti ya Kisumu wana jukumu la kuhakikisha kuwa taka zinazopatikana kwenye maeneo ya makaazi zinaondolewa na kupelekwa kwenye maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kutupa taka.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akizungumza kwenye kikao cha Sauti ya Jamii katika eneo la Manyatta kilichowaleta pamoja wakaazi wa mitaa ya mabanda jijini Kisumu, afisa mpanga ratiba wa Obunga Residents Association Daniel Ayieko, alilalama kuhusu mirundiko ya taka, hasa kwenye mitaa ya mabanda.

“Kila mara tunafanya usafi kwenye mitaa yetu, lakini changamoto tunayopta ni kwamba gari la serikali ya jimbo la kuzoa taka halijii kuchukua taka,” alisisitiza Ayieko.

Naye afisa mpanga ratiba wa Manyatta Residents Association Dickens Ochieng, amesema eneo hilo linashuhudia changamoto za kudumisha usafi, hasa ukosefu wa vyoo.

Alisema kuwa baadhi ya wenyeji wamelegeza kamba kwa kutotilia maanani usafi, akionyesha hofu ya kutokea kwa mkurupuko wa magonjwa yanayosababishwa na uchafu.

Afisa wa mawasililiano katika shirika hilo Suleiman Okoth, alisisitiza kuhusu umuhimu wa wadau wote katika sekta ya usafi na

Aidha, alitoa wito kwa wananchi kuisoma katiba ndiposa wafahamu haki zao, ili washinikize kupokea huduma bora kutoka kwa serikali ya kitaifa na ile ya kaunti.

Kikao hicho kiliandaliwa na shirika la Umande Trust, lenye makao yake jijini Kisumu.