Maafisa wa trafiki katika Kaunti ya Mombasa wamenazisha msako dhidi ya wahudumu wa matatu wasiofuata sheria za barabarani.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Utingo 15 pamoja na madereva 11 tayari walitiwa mbaroni siku ya ijumaa na kufikishwa mahakamani kwa kukiuka sheria za trafiki.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini mwake siku ya Ijumaa, kamanda wa trafiki mjini Mombasa Shem Omolo alisema kuwa wahudumu hao walikamatwa kwa makosa tofauti kama vile kukosa leseni, sare za utingo na madereva, kusajili upya leseni za kuendesha gari pamoja na kukosekana kwapicha zao kwenye magari..

“Utingo ishirini pamoja na madereva wanane walifikishwa mahakamani siku ya Alhamisi kwa kukiuka sheria za barabarani. Operesheni hiyo itaendelea hadi pale wahudumu wote wa matatu wanaohudumu mjini Mombasa watakapofuata sheria za trafiki,” alisema Omolo.

Haya yanajiri wiki chache tu baada ya wahudumu kadhaa wa tuktuk kupelekwa mahakamani kwa makosa kama hayo.