Maafisa wa usalama Kaunti ya Mombasa wametakiwa kutowatia mbaroni wavuvi wanapoendeleza shughuli zao baharini.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza siku ya Jumatano wakati wa maadhimisho ya sherehe za Madaraka katika uwanja wa Tononoka, Mwakilishi wa wanawake Kaunti ya Mombasa Mishi Mboko aliwasihi polisi kutowahangaisha wavuvi hao.

“Ningependa kuwahimiza maafisa wa usalama kutowahangaisha wavuvi ikizingatiwa kuwa wao sio wahalifu bali wanatafuta riziki yao,” alisema Mboko.

Kauli hii inajiri baada ya wavuvi kulalama kuwa wanahangaishwa na maafisa wa usalama wanapokuwa wanaendeleza uvuvi wao.

Wakati huo huo, ameitaka serikali ya kaunti kuwanunulia wavuvi vifaa vya kisasa vitakavyowasaidia katika kuendeleza shughuli zao.