Mwenyekiti wa wanabiashara katika kaunti ya Kisii Benjamin Onkoba amewalaumu maafisa wa polisi kwa kuchukua muda mrefu kabla ya kutuliza labsha zilizofanywa na wanafunzi wa Taasisi ya Gusii Institute of Technology.
Akiongea na waandishi wa habari siku jumanne katika mji wa Kisii Onkobo aliwalaumu vikali maafisa wa polisi kwa kuzembea kazini mwao.
“Maafisa wa polisi wangefika wakati walijulishwa kuhusu ghasia hizo wangeweza kuzuia uharibifu huo,” alisema Onkoba.
Onkoba aliwalaumu vikali maafisa wa polisi kwa kutofanya kazi yao vinavyostahili.
Aidha afisa huyo alisema kuwa maafisa wa usalama walichukuwa zaidi ya masaa 18 kuja kuwadhimbiti wanafunzi hao.
“Mali ya wanabiashara iliharibiwa na wanafunzi waliokuwa wameasi.Askari wangefika kwa wakati wangeweza kuzuia uharibifu huo,” asema Okoba.
Onkoba aliomba serikali kuhakikishia wanabiashara usalama wao pamoja na ule wa biashara zao.
Wakati uo huo Onkoba aliomba wanachi kutotumiwa na baadhi ya wanasiasa kuanza vurugu.
“Naomba wakazi waeneo hili wasije wakatumiwa na wanasiasa kutenda mambo ambayo yanawaathiri wenzao,”aliongeza Onkoba.