Maafisa wawili wa usalama pamoja na raia wawili wamefikishwa mahakamani kwa kosa la utekeji nyara.
Aliyekuwa mwanajeshi Nassiri Otieno, Timothy Ngenya ambaye ni afisa wa polisi wa cheo cha koplo, Hamisi Juma na Rosemary Ngina ambaye anasemekana kuwa mke wa afisa mmoja wa upelelezi wanadaiwa kumteka nyara Abdalla Rashidi mnamo Julai 6 mwaka huu katika eneo la Harambee huko Likoni.
Wanne hao pia wanakabiliwa na mashtaka ya kuitisha fidia ya shilingi elfu 70 kutoka kwa wazazi wa Rashid ili wamuachilie huru.
Wakati huo huo, afisa Ngenya anakabiliwa na shtaka la kupatikana na pakiti nne za heroine zenye thamani ya shilingi mia nane, pamoja na misokoto kumi ya bangi yenye thamani ya shilingi mia mbili.
Washukiwa hao walikanusha mashtaka hayo mbele ya Hakimu mkuu Julius Nang’ea.
Wanne hao waliachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni moja kwa kosa la utekeji nyara.
Kesi yao itatajwa Julai 20, mwaka huu.