Waziri wa afya katika kaunti ya Kisii Sarah Omache amesema visa vya maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi vimepungua katika eneo hilo.
Kulingana naye, ripoti ya mwaka jana ilionyesha kuwa maambukizi ya ugonjwa huo wa ukimwi katika kaunti ya Kisii ilikuwa asiliama nane nukta tisa ilihali mwaka huu, maambukizi hayo yamepungua hadi asilimia tano na kusema kuna imani ya kurudisha asilimia hiyo ya maambukizi hadi asilimia sifuri.
Akizungumza siku ya jumanne katika uwanja wa michezo wa Gusii mjini Kisii wakati wa kusherekea siku ya ugonjwa wa ukimwi duniani, waziri Omache alisema maambukizi ya ugonjwa huo yamepungua kwa asilimia kubwa.
“Katika mwaka huu wa elfu mbili na kumi na tano, maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi yamepungua kutoka asilimia nane unkta tisa hadi asilimia tano na nina imani kuwa maambukizi hayo yatarudi hadi asilimia sifuri,” alisema bi Omache.
Aidha,Omache aliwashauri watu kujua hali zao za afya kwa kujitokeza kupimwa kwani mtu anapojua hali yake anawekwa katika ratiba ya kupokea dawa za kupunguza makali ya virusi iwapo anapatikana ana ugonjwa huo na lishe bora.
Wale amabo watapatikana hawana virusi hivyo, watashauriwa jinsi ya kuishi vyema na kijukinga na maambukizi.