Utafiti uliofanywa na Baraza la kitaifa la kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi NACC, umebaini kuwa asilimia 46 ya maambukizi mapya ya ugonjwa wa ukimwi nchini ni miongoni mwa vijana.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mshirikishi wa mipango anayesimia vijana katika baraza hilo Jacquline Ndaachi amesema kuwa hatua hiyo imechangiwa pakubwa na jamii kutowahusisha vijana katika kampeni za hamasa kuhusiana na ugonjwa huo.

Akiongea katika kongamano la kuzindua upya sera za kukabiliana na ugonjwa huo nchini Bi Ndaachi alisema kuwa vijana wa umri wa kati ya miaka 10 hadi 25 wako katika hatari zaidi ya maambukizi.

"Katika utafiti wetu tumebaini kuwa vijana wa umri wa miaka 10 hadi 25 wako katika hatari ya kuambukizwa virusi vya ukimwi kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya ugonjwa huo,” alisema Ndaachi.

Bi Ndaachi amependekeza taasisi mbalimbali pamoja na wazazi kuchukua jukumu la kuongea na vijana kuhusiana na maswala ya ngono.

Mshirikishi huyo alisema kuwa maambukizi hayo yameongezeka hadi asilimia 46 licha ya kuwa asilimia 29 mwaka wa 2014.