Maandano ya mrengo wa upinzani nchini Cord kushinikiza makamishina wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini (IEBC) sio suluhu ila kufuata sheria iliyoko ili kuwanabandua.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakizungumza siku ya Jumapili mjini Kisii chama cha wazee wa jamii hiyo chini ya mwavuli wa 'Jubilee Storm Amani Kenya' kikiongozwa na Thomas Guto walisema mrengo wa Cord unafaa kutumia sheria kuwaondoa makamishina wa IEBC kwani makamishina hao walipokezwa afisi hiyo kisheria. 

Aidha, walisema mbuni ambayo mrengo wa Cord unatumia kwa njia ya maandamano kulazimisha makamishina hao kuondoka ni jambo ambalo halistahiki hata kidogo.

“Viongozi wa Cord wanafaa kutumia sheria kuwaondoa afisini makamishena wa IEBC wala sio kutumia kifua maana huo ni sawa na ukiukaji wa sheria,” alisema Guto.

Wakati huo huo, wazee hao waliomba jamii ya Gusii kutoungana na Cord kufanya maandamano katika afisi za IEBC katika sehemu mbalimbali nchini kwa kusema ni kutumiwa vibaya huku wengine wakijitakia mema.

“Watoto wa viongozi wale wanaongoza maandamano wako nyumbani wakifanya yao sasa wanatumia wengine kujeruhiwa," alisema Guto.

"Jamii ya Gusii tumekataa na watoto wetu hawatajiunga kwenye maandamano,” aliongeza Guto