Naibu Gavana wa Kisii Joash Maangi amewaomba wazazi kuwawekea watoto wao usalama haswa msimu huu wa mvua nyingi inyoendelea kushuhudiwa nchini Kenya.
Maangi alihofia kuwa huenda watoto wengi wakasombwa na mfuriko wakati wanapoenda shule.
Naibu gavana aliyasema haya baada ya mototo wa umri wa miaka 12 kutoka sehemu ya Daraja Mbili kusombwa na mafuriko Jumatano wiki hii alipokuwa aki toka shuleni kuelekea nyumbani.
Mwili wa mwanafunzi huyo wa Darasa la nne katika shule ya kibinafsi ya Bosire ulipatikana Alhamisi asubuhi katika mto wa Riana.
“Nawaomba wazazi kuwa maakini haswa msimu huu wa mvua nyingi kwa kuwalinda watoto wao wanapotoka na kuenda shuleni kama njia moja ya kuwahakikishia usalama kutokana na mafuriko yanaotokana na mvua,” alishauri Maangi.
Katika ujumbe wa naibu gavana Maangi kwa familia ilio aathiriwa, aliwapa pole na kuwatakia heri wakati wanapoomboleza kifo cha ghafla cha mototo wao.
Haya yanajiri huku wakaazi wa Nyabite katika eneo bunge la Mugirango Maghari, Kaunti ya Nyamira wakilalamikia utepetevu wa kutengeneza daraja katika sehemu hiyo vilivyovunja kingo zake kutotkana na mafuriko, ambayo wanahoji imepelekea watu wengi kunusurika kifo kwa kusombwa na maji.