Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Naibu gavana wa kaunti ya kisii Joash Maangi amewarai viongonzi wa humu nchini wakiwemo magavana, manaibu gavana na wananchi kuunga mkono mradi wa pesa mashinani ili pesa ziongezwe mashinani na kuleta maendeleo.

Akiongea siku ya Jumatatu katika mji wa kisii, naibu huyo alisema serikali za ugatuzi hushughulikia mambo mengi na pesa hizo zafaa ziongezwe zaidi ili maendeleo yaweze kufanyika kupitia serikali za ugatuzi. 

“Sekta ya afya iko chini ya uongozi wa kaunti na sekta hiyo ndio inahitaji pesa nyingi ili kuridhisha yale yanahitajika kufanywa katika sekta hiyo. Naomba pesa ziongezwe mashinani ili kila kitu kufanyika kikamilifu,” alisema Maangi. 

“Kusema tunahitaji pesa kongezwa kwa serikali za kaunti haimanishi tunazozana na serikali kuu. Tunahitaji pesa hizo kuwa nyingi ili tuweze kufanya maendeleo zaidi,” aliongeza Maangi.

Aidha, naibu huyo ambaye pia ni mwenyekiti wa manaibu gavana nchini aliomba magavana na manaibu wao kuwatumikia wananchi vilivyo na kuwaomba kushirikiana pamoja na kuunga mkono mradi huo wa pesa mashinani.

Wakaazi wa kaunti hiyo walisema kuwa wanahitaji serikali za kaunti kufanya maendeleo kwani ndizo serikali ambazo ziko karibu na wakaazi.

“Tusipofanyiwa maendeleo na serikali ya kaunti basi hatutaona maendeleo. Naunga mkono mradi huo wa pesa mashinani,”alisema Peter Bibao, mkaazi wa kisii.