Naibu gavana wa kaunti ya Kisii Joash Maangi amewataka wazazi, walimu, washikadau na wanafunzi kushirikiana kuinua viwango vya masomo.
Akizungumza siku ya Ijumaa katika mji wa Kisii wakati hafla ya walimu wakuu wa shule za upili ilikuwa ikifungwa baada ya kufikia mwisho, Maangi aliomba wazazi kushirikiana na walimu ili wanafunzi kupita katika mitihani wa kitaifa.
“Sharti elimu izingatiwe maana itasaidia watoto wetu siku zijazo, na ninawaomba wahusika wote kushirikiana pamoja ili viwango vya masomo kuinuka katika eneo la Kisii,” alisema Maangi.
Maangi pia aliwaomba wazazi kufanya na kutekeleza yale yanahitajika kwa upande wao ili wasiwaachie walimu pekee kuhusika na watoto, na kuomba kusaidiana pamoja ili wanafunzi kupita katika mitihani
“Lazima kila upande uwe na motisha iwe ni upande wa wazazi, walimu, washkadau na wanafunzi na viwango vya elimu Kisii vitaonekana kuinuka Zaidi na kunawiri milele,” aliongezea Maangi
“Jambo nzuri ni motisha kati ya wahusika wote na wakati wa mavuno kila upande utafurahia, si upande wa walimu pekee, hata kaunti nzima itafurahi baada ya kufanya vizuri kwa masomo,” alidokeza Maangi.
Walimu wakuu hao walifurahishwa na ombi hilo la naibu gavana kwa kuomba wazazi kushirikiana na walimu, na sio kuwaachia walimu mzigo.
“Mie naona ni vizuri kushirikiana pamoja na wazazi wazituajie walimu pekee kwa wanafunzi lakini tukishirikiana wanafunzi watapita mitihani,” alihoji Zablon Nyakundi, mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Nyagonyi.