Wataalamu wa hali ya anga na rasilimali ya bahari wameonya kuwa makavazi yaliyo karibu na bahari, yako katika hatari ya kuzama baharini, kutokana na mabadiliko ya hali ya anga na kuinuka kwa viwango vya bahari.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akiongea baada ya kuzuru makavazi ya Fort Jesus mjini Mombasa siku ya Jumatatu, mkurugenzi mkuu katika idara ya makavazi nchini, Mzalendo Kibunjia, alisema kuwa walipokea ilani hii baada ya utafiti kufanywa karibu na makavazi hayo.

“Ningependa kutoa wito kwa serikali kutenga fedha katika bajeti yake kuboresha makavazi hayo ili kuzuia hatari zozote. Huenda sekta ya utalii ikaathirika iwapo hatua hizo hazitachukuliwa,” alisema Kibunja.

Mkurugenzi huyo pia alisema kuwa huenda jambo hilo likahatarisha maisha ya binadamu kwa kuwa ikizama iwapo watu wako karibu, huenda ikazama nao.

Makavazi ambayo yametajwa kuathirika na hali hii ni pamoja na makavazi ya Fort Jesus, jiwe kuu la Vasco Dagama na majengo ya uingereza yaliyo Vanga.