Kutokana na ongezeko la mabango ya waganga nchini, bodi ya ukaguzi wa filamu nchini imepiga marufuku mabango ya waganga yanayotundikwa kila mahali yakinadi kazi zao.
Mabango hayo hutumika sana na kijitangaza kwamba ni daktari wa mapenzi, kuvuta walio mbali na hata kutafutia watu kazi.
Siku ya Jumanne, afisa mkuu mtendaji wa bodi hiyo Ezekiel Mutua alisema kuwa watawachukulia hatua wenye kuweka mabango ya matangazo ya matibabu ya kienyeji na mengine ambapo huwa ni ya urongo.
Aliongeza kuwa bodi hiyo itashirikiana na serikali za Kaunti ili kuhakikisha hakuna mabango ya kukera .