Madaktari kutoka Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Kisii wameunga maseneta mkono kwa kusema kuwa watahakikisha kuwa sekta ya afya itasimamiwa na serikali za kaunti.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akiongea na waandishi wa habari hii leo ofisini mwake, daktari mkuu katika Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Kisii, Geofrey Ontomu, alisema kuwa wanaunga mkono azimio la waseneta kufanikisha sekta ya afya kusimamiwa na serikali za kaunti ili kufikia mwanaichi wa kawaida.

Kulingana na Ontomu, tangu serikali za ugatuzi kuanzishwa, kaunti ya Kisii ikiwa mojawapo sekta hiyo imekuwa na mabadiliko makubwa katika hospitali ya Kisii na wanaichi wanefaidika pakubwa.

“Tangu serikali ya Kaunti ianze kusimamia sekta ya afya kuna mengi ambayo yamefikiwa na wanainchi wa kawaida wamefaidika pakubwa kwa kupata hudumu bora,” alisema Daktari Ontomu.

Serikali ya Kaunti ya Kisii imepiga hatua kubwa katika sekta ya afya kwa hivyo madaktali hao wanaomba serikali kuu kutoa pesa kwa serikali za kaunti ili waweze kufanya zaidi.

Aidha,Daktari Ontomu amesema kuwa tangu mvutano uanze kati ya serikali kuu na serikali za kaunti kuhusu ni nani anastahili kusimamia viwango vya sekta hiyo  vimepungua katika hospitali ya Kisii.

Kwingineko, kutokana na kupunguzwa kwa kiasi cha pesa ambazo kaunti ya kisii ilipokea kutoka kwa serikali kuu kutoka million 211 hadi million 83 miradi mingi katika hospitali hiyo imekwama kuendelea haswa ujenzi wa baadhi ya nyumba.

“Kutokana na kupunguzwa kwa kiasi hicho cha pesa miradi nyingi imepungua kwa hivyo tunaomba serikali kuu kukubali serikali za kaunti kusimamia sekta hiyo ya afya kwa kuwa ni mengi wamefanya  kwa kipindi kichache wakiwa uongozini,” aliongezea Ontomu.