Washikadau wa hospitali kuu kaunti ya kilifi wamebaini kuwa baadhi ya wahudumu wa afya katika hospitali mbalimbali za kiserikali ndio wezi wakubwa wa dawa za hospitali za umma.
Afisa mkuu wa wizara ya Matibabu Daktari Timothy Malingi amesema kuwa katika uchunguzi uliofanywa na sekta ya afya eneo hilo, wanaomiliki hospitali za kibinafsi ni madaktari wa hospitali za umma hali ambayo anasema imewafanya kuiba dawa na kupeleka katika hospitali zao.
Uchunguzi huo unajiri baada ya maafisa wa afya kuifunga hospitali moja mjini kilifi baada ya kubainika kuwa ilikuwa ikiendeshwa kinyume cha sheria.
Aidha Malingi ameghadhabishwa na hatua hiyo huku akisema kuwa wananchi haswa katika maeneo ya mashinani wamekuwa wakikosa dawa katika zahanati za umma na kuelekezwa kwenye hospitali za kibinafsi ambazo wanazimiliki.