Madereva wa malori ya masafa marefu siku ya jumapili walitoa masikitiko yao kutokana na wizi kwenye barabara kuu ya Maai Mahiu-Naivasha.
Dereva mmoja aliuawa siku ya Ijumaa katika barabara hiyo yenye shughuli nyingi.
Madereva hao walisema kuwa eneo la Longonot na Chechnia ndio maeneo hatari kabisa ambako kila wiki kisa cha wizi huripotiwa.
Dereva mmoja, Ali Juma, aliwahimiza polisi kuangazia swala hilo kwa haraka kabla ya maafa mengine kushuhudiwa.
“Tunasikitika sana na uwizi ambao unalenga matrela haya yetu katika barabara hii na tunawahimiza maafisa wa polisi kupambana na majambazi hawa wanaotuangaisha kula kuchao.” Alisema Bw Juma.
Polisi katika siku za hivi karibuni, wamekuwa wakiwashtumu baadhi ya madereva hao dhidi ya kujiunga na majambazi na kutekeleza wizi katika matrela hayo.