Majuma machache tu baada ya kampuni ya uchukuzi ya Uber yenye kitovu chake nchini Marekani kupunguza ada zake jijini Mombasa kufuatia ushindani mkali unaoshuhudia katika biashara ya uchukuzu, kampuni hio imekumbwa na kitendawili kipya.

Share news tips with us here at Hivisasa

Hii ni baada ya madereva watatu wanaofanyakazi na kampuni jiyo jijini Mombasa kufikishwa mahakamani kwa kosa la kuegesha texi zao bila vibali katika uwanja wa ndege wa Moi ulioko maeneo ya Changamwe wiki jana.

Washtakiwa hao, Lewis Machuki Maragia, Martin Nginge na Charles Wangudi Mwangi walikanusha madai hayo mbele ya hakimu mkuu Tersiah Matheka, siku ya Jumanne.

Aidha, washtakiwa hao wanadaiwa kutomiliki vibali vya kuwaruhusu kuegesha magari katika uwanja huo wa ndege.

Mahakama iliwaachilia kwa bondi ya shilingi 20, 000 kila mmoja au mdhamini wa kiasi sawa na hicho.

Kesi hio inatarajiwa kusikizwa Desemba 1.