Tabia ya baadhi ya medereva kuendesha magari yao kwa mwendo wa kasi na pia kubeba abiria kupita kiasi ni miongoni mwa maswala ambayo yamelaumiwa kwa ongezeko la ajali barabarani hamu nchini.
Akiongea mjini Eldoret, naibu mkurugenzi wa halmashauri ya uchukuzi na usalama nchini Cosmas Ngesa alikashfu tabia hiyo, ambayo alisema imekithiri miongoni mwa madereva.
Ngesa alikuwa akizungumza kwenye mkutano wa uhamasisho ulioleta pamoja wahudumu wa matatu mjini Eldoret.
Vle vle, alisema kwamba utafiti unaonyesha kuwa mwendo wa kasi ni mojawapo ya sababu zinazosababisha ajali nyingi sana.
Naibu huyo alitoa onyo kali kwa madereva wanaokiuka sheria za barabarani, huku akisema atakayepatikana atachukuliwa hatua zifaazo za kisheria.
Aliongeza kuwa mamlaka hiyo imeungana na polisi wa trafiki kufanya utafiti kwa kutumia teknolojia za kisasa, ili kukabili tabia potovu za waendeshaji magari barabarani.
Makampuni yanayotoa vidhibiti mwendo bandia pia hayakusazwa, kwani Ngesa alisema mamlaka hiyo itawachukulia hatua kali na hata kufutilia mbali vyeti vyao vya kazi.