Takriban shilingi bilioni 5.3 zimetolewa na hazina ya uwezo katika maeneo bunge 289 kwa minajili ya kustawisha akina mama na vijana.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akizungumza kwenye mkutano uliondaliwa katika chuo cha leba cha Tom Mboya jijini Kisumu, mkurugenzi mkuu wa Uwezo Wilfred Buyema amesema kuwa eneo bunge moja tu; Kisumu Rural ambalo halijapokea fedha hizo kwa sababu haijatimiza masharti yaliyowekwa.

Mboya ameongeza kuwa ipo haja ya serikali kuongeza bajeti ya hazina hiyo, ili kufanikisha utendakazi wake hasa kwa kuhamasisha umma.

Aidha, ametoa tahadhari kwa wale ambao wamepokea fedha hizo dhidi ya kuzitumia katika sherehe za krisimasi na mwaka mpya, na badala yake watumie katika miradi za kujiendeleza.

Kwa upande wake, mwenyekiti wa hazina ya uwezo eneo bunge la Gilgil kaunti ya Nakuru Steven Sarikoki amenyoshea kidole cha lawama baadhi ya wafanyikazi wa umma wanaohusika kuhujumu hazina hiyo.

Hazina iyo ilitengwa rasmi kuwasaidia vijana, kina mama na walemavu ili kujiendeleza kimaisha.