Kifo cha Mama Lucy Muthoni Kibaki bila shaka ni pigo kubwa kwa nchi.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Marehemu alikuwa mama mwenye moyo wa huruma na kama mke wa aliyekuwa wa rais Mwai Kibaki, aliipa uongozi wake mtazamo mpya.

Jinsi alivyotekeleza wajibu wake kama mama wa taifa ni mfano wa kuigwa. 

Uaminifu wake kwa familia yake, mme wake pamoja na nchi hii ni jambo ambalo limefanya viongozi wengi kumtambua kama mama aliyejivunia kuwa mkenya. 

Alishinda wengi kwa kujiamini kwake, alikua mwanaharakati wa mayatima walioachwa baada ya familia zao kuangamia kwa janga la ukimwi. 

Huko kujitolea kwake kulifanya hospitali ya wilaya ya Embakasi (Nairobi), kubadilishwa jina na kuitwa Mama Lucy Kibaki Hospital kama kumbukumbu kwake.

Hospitali hiyo inahudumia zaidi ya watu millioni mbili huko Eastlands. 

Pia alikua kifua mbele kupigania kuelimishwa kwa mtoto wa kike na haki za wanawake. 

Kuanzishwa kwa shule ya upili ya wasichana ya Starehe Girls Centre iliwezekana kupitia kwa bidii yake ya kutaka kuona watoto werevu wa kike wakinufaika bila kuzingatia hali duni ya maisha ya familia zao.

Ingawa ametuacha, Mama Lucy ataendelea kuishi katika maisha yetu kama Wakenya.