Washika dau katika sekta ya matatu kaunti ya Nakuru wamekaribisha hatua ya mamlaka ya usafiri na usalama nchini, NTSA kuyaondoa magari madogo yanayo jihushisha na usafiri wa umma.
Akizungumza na wanahabari, mwenyekiti wa wamiliki wa matatu za Central Rift katika jimbo la Nakuru Stephen Muli alisema magari hayo yamechangia pakubwa katika kudorora kwa biashara ya matatu.
''Sisi kama waathiriwa wakuu tutafanya kila juhudi kuhakikisha kuwa sheria mpya ya NTSA imeidhinishwa haraka ipasavyo,'' alisema Muli.
Muli alisema kuwa magari ya aina hiyo yamechangia pakubwa katika kusababisha ajali barabarani huku akiwataka washikadau wote kushirikiana katika kufanikisha sheria hiyo.
Sheri hiyo pia imeungwa mkono na waziri wa usafiri katika Kaunti ya Nakuru, Maina Kairu akisema kuwa sheria hiyo itaunganisha sekta ya usafiri nchini.