Mshirikishi mkuu wa ukanda ya Pwani Nelson Marwa amesema magari yote ya usafiri yanayo hudumu katika barabara ya Mombasa-Lamu yatapewa ulinzi mkali, ili kuzuia visa vya uvamizi wa ugaidi msimu huu wa likizo.
Marwa amesema idara ya usalama iko macho kutoa ulinzi wa kutosha hasa wakati huu ambapo wageni wanamiminika eneo la Pwani kwa likizo za krismasi na mwaka mpya.
“Polisi watakuwa wakitoa ulinzi wa kutosha kwa magari hayo, ili wasafiri wawe salama,” alisema Marwa.
Ameongeza kuwa usalama umeimarishwa pia katika maduka makuu pamoja na afisi za serikali kote Pwani.
“Kila duka na afisi za serikali zitalindwa mara dufu msimu huu wa sherehe ili kuepuka mashambulizi,” alisema Marwa.
Ikumbukwe maeneo ya Mombasa na Lamu yamekuwa yakishambuliwa na wanamgambo wa al-shabab baada ya wanajeshi wa Kenya kuenda Somalia kwa operetion Linda nchi mnamo Oktoba mwaka 2011.