Kamishna wa Kaunti ya Mombasa Mohamed Maalim amewataka maafisa wa usalama kuchungunza magari ya viongozi wote wa serikali kuu pamoja na zile za kaunti.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Maalim ametoa muongozo huo baada ya idara ya ujasusi kutoa ripoti kuwa magaidi wameanza kutumia magari yenye nambari za usajili za GK na UN.

Akizungumza siku ya Jumanne wakati wa maadhimisho ya sherehe za Madakara katika uwanja wa Tononika jijini Mombasa, Maalim alisema ipo haja ya kuimairisha usalama ili kutibua mipango ya magaidi.

Maalim amewataka viongozi hao kushirikiana na walinda usalama wanapotekeleza shughuli zao za ukaguzi wa magari hayo.