Magavana wanafaa kusaidiwa pakubwa na wananchi katika kufanikisha uongozi kwani wao si malaika.

Share news tips with us here at Hivisasa

Ni kauli yake mwanaharakati Masese Kemunche kutoka shirika LA Centre for Enhancing Democracy and Good Governance CEDGG.

katika mahojiano kwa njia ya simu Jumanne asubuhi, Kemunche alisema kuwa wananchi wana wajibu wa kuhakikisha katiba inatekelezwa kikamilifu.

Aliongeza kuwa ili ugatuzi kufaulu, mwananchi anafaa kuwa macho kuwakosoa magavana na wala sio kuwa vibaraka tu wa kusifu viongozi.

"Ni vyema wananchi watambue kwamba magavana sio malaika WA kufanya mambo inavyotakikana bali wakikosea wanafaa kurekebishwa na huo ndio ufanisi wa ugatuzi" Masese alisema.

Wakati huo huo, alizitaka serikali za kaunti kuhakikisha kwamba zinawahusisha kikamilifu wananchi katika uongozi.