Magavana kutoka ukanda wa Pwani katika mkutano wa awali. [Photo/ plus.google.com]

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Magavana wa Pwani wameapa kuungana ili kufanikisha maazimio ya Jumuia ya Kaunti za Pwani.

Haya yaliafikiwa kwenye mkutano mjini Mombasa uliowaleta pamoja magavana wote sita wa Pwani.

Magava hao walisema kuwa watazika tofauti zao za kisiasa ili kuleta maendeleo kwa wananchi.

Aidha, waliahidi kushirikiana kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta za kilimo, ufugaji, utalii na uvuvi.

Gavana wa Kaunti ya Kilifi Amason Kingi alisema kuwa ipo haja ya jumuia hiyo kuwekeza katika utafiti wa kimaendeleo ili kuiga mfano wa nchi zilizoendelea.

Kingi amezitaka kaunti hizo kuweka raslimali zao pamoja ili kuhakikisha jumuia hiyo inaafikia maazimio yake.

“Tutajitahidi kuwekeza katika miradi ya maendeleo ili tuweze kufaulu,” alisema Kingi.

Kwa upande wake, Gavana wa Mombasa Hassan Joho alisema kuwa jumuia hiyo imekumbwa na changamoto chungu nzima ikiwemo mwingilio wa kisiasa.

Hata hivyo, alisema kuwa iwapo viongozi na wakaazi watahusihswa kikamilifu, jumuia hiyo itaimarika na kuchukua mwelekeo mpya.

“Changamoto ziko lakini tutazikabili vilivyo,” alisema Joho.