Magavana wa Pwani wametakiwa kueleza kuhusu kiwango cha fedha ambacho wametumia katika kuendeleza harakati za kuunda kwa jumuiya ya kaunti za pwani.
Haya yanajiri baada ya kuzuka tetesi kuwa huenda pesa hizo zimefunjwa.
Mbunge wa Kilifi Kaskazini Gideon Mung’aro, alisema siku ya Jumanne, kuwa huenda zikawa zimefujwa hasa katika safari na maandalizi ya mikutano ya maafisa wa serikali za kaunti na magavana.
Aidha, alieleza kuwa lazima pesa ya mlipa ushuru iheshimiwe kwa kuendeleza miradi badala ya kuanzisha mpango ambao hautawasaidia wapwani.