Mahakama ya Mombasa. Picha: Haramo Ali/ hivisasa.com
Mahakama ya Mombasa inatarajiwa kutoa uamuzi juma lijalo wa iwapo raia 18 wenye asili ya Kisomali watarudishwa kwao baada ya kuingia nchini kinyume cha sheria.
Hii ni baada ya ripoti iliyotolewa na idara ya uhamiaji kuonyesha kuwa raia hao walikimbilia humu nchini kutoka Somali kufuatia ukosefu wa usalama.Ripoti hiyo iliyowasilishwa mbele ya Hakimu Julius Nangea inaonyesha kuwa vita vya ndani kwa ndani katika jamii ya Gulguud ndivyo vilivyowafanya raia hao kutoroka makwao.Uamuzi wa kurudishwa kwao utatolewa Machi 15, 2017.Watatu kati yao ni watoto wenye chini ya umri wa miaka 10, wasichana 12 na wavulana sita wanaodaiwa kupatikana katika eneo la Mwembe Tayari mnano Machi 4.