Jengo la mahakama ya Mombasa. [Photo/The Star]

Share news tips with us here at Hivisasa

Mahakama kuu ya Mombasa itatao uamuzi wa iwapo itatupilia mbali kesi ya kupinga ushindi wa gavana wa Mombasa Hassan Joho mwishoni mwa mwezi huu.

Ikumbukwe Sarai alipata kura 44,000 huku Joho akiibuka mshindi na kura 220,000.

Kesi hii iliwasilishwa mahakamani na aliyekuwa seneta wa Mombasa Hassan Sarai ambaye alishindwa kwenye kiti cha ugavana kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti.

Joho aliwasilisha ombi la kutupiliwa mbali kwa kesi hiyo kwa kusema kuwa haina msingi wowote wa maana,ikizingatiwa alichaguliwa  kihalali.

Mawakili wa Joho, wakiongozwa na Mohamed Balala wameitaka mahakama kutupilia mbali kesi kwa kusema kuwa Joho alichaguliwa kihalali.

Naye wakili wa Sarai, Yusuf Aboubakar ameitaka mahakama kututupilia mbali kesi hiyo kwa kusema kuwa ombi lililowasilishwa na Joho halina msingi wowote.

Jaji Lydia Achode anatarajiwa kutoa uamuzi wake Oktoba 24,10,2017.