Mahakama kuu ya Mombasa imeahirisha kutoa hukumu ya mshukiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwenyekiti wa CIPK Sheikh Mohamed Idris.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mshukiwa huyo, Mohamed Soud, anadaiwa kuhusika katika mauaji ya marehemu Sheikh Mohamed Idris, mnamo Juni 10, 2014 katika eneo la Likoni.

Siku ya Alhamisi, Jaji Martin Muya alisema kuwa hajamaliza kuandika hukumu hiyo na kupendekeza kuitoa tarehe Aprili 15 mwaka huu.

Mnamo Januari 2, 2016, mke wa mshukiwa huyo, Aisha Khalifa, alitokwa na machozi alipokuwa akielezea mahakama jinsi alivyopigwa kofi na maafisa wa polisi waliokuwa wamemtia mbaroni mumewe Mohamed Soud.

Soud kwa upande wake aliwalaumu maafisa wa usalama kwa kumhusisha na mauaji hayo pamoja na umiliki wa bunduki na kilipuzi, kwa kusema kuwa hana ujuzi wa kutumia silaha hizo hata kidogo.

Mkewe alisisitiza kuwa hakukuwa na vilipuzi na bunduki katika godoro lao kama inavyodaiwa na polisi.