Jengo la Mahakama ya Mombasa.[Picha/ the-star.co.ke]

Share news tips with us here at Hivisasa

Mahakama ya Mombasa inatarajiwa kutoa uamuzi wa iwapo itatupilia mbali kesi ya ufujaji wa fedha za CDF inayomkabili aliyekuwa mbunge wa Lamu Magharibi.Hii ni baada ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma nchini kuwasilisha ombi la kumuondolea Julius Ndegwa mashtaka hayo wiki iliyopita.Ombi hilo liliwasilishwa katika Mahakama ya Mombasa na naibu mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma tawi la Mombasa Alexendra Muteti.Muteti alipokea agizo hilo kutoka kwa afisi kuu ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma nchini Keriako Tobiko, baada ya kuhisi ushahidi unaozidi kutolewa ni hafifu.Ndegwa alishtakiwa pamoja na maafisa wengine sita wa kamati ya hazina ya CDF ya eneo bunge la Lamu Magharibi.Wasaba hao wanadaiwa kushirikiana kuiba shilingi milioni mbili kutoka hazina hiyo ya CDF.Tayari zaidi ya mashahidi kumi wametoa ushahidi wao kuhusiana na kesi hiyo.Uamuzi huo utatolewa leo (Alhamisi Oktoba 19, 2017).