Mahakama ya Mombasa inatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu iwapo uchunguzi wa mvulana anayedaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na wanajeshi eneo la Mtongwe utafanyika au la.

Share news tips with us here at Hivisasa

Hii ni baada ya familia ya mwendazake Suleiman Athuman, kuwasilisha ombi la kutaka kufanyika uchunguzi huo siku ya Jumanne, ili kubaini waliohusika katika mauaji ya mtoto wao.

Hakimu Henry Nyakweba alisema kuwa amepokea ombi hilo na kuwa atatoa uamuzi kabla ya mwisho wa wiki.

“Nitatoa uamuzi wa ombi hilo siku ya Alhamisi,” alisema Hakimu Nyakweba.

Mwili wa Suleiman Athuman ulipatikana karibu na kambi ya jeshi la Mtongwe mnamo Januari 11 mwaka 2015, huku ukiwa na majereha ya risasi.