Mahakama kuu ya Mombasa imesimamisha dhamana ya Haniya Saggar, mjane wa marehemu Sheikh Aboud Rogo kwa muda usiojulikana baada ya afisi ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma kukata rufaa dhidi ya dhamana hiyo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akitoa uamuzi huo, Jaji Dora Chepkwonyi aliagiza kesi hiyo iliyokuwa ikiendelea katika Mahakama ya Shanzu kusimamishwa hadi pale rufaa iliyowasilishwa mbele yake itakapokamilika.

“Hakuna kuendelea na kesi hiyo tena katika Mahakama ya Shanzu hadi nitakapo maliza kusikiza rufaa hii,” alisema Hakimu Chepkwonyi.

Siku ya Alhamisi, afisi ya mkurungenzi mkuu wa mashtaka ya umma tawi la Mombasa, ikiongozwa na mwendesha mashtaka Jami Yamina, ilipinga kigezo kilichotumiwa na Mahakama ya Shanzu kwamba Saggar hawezi kutoroka kwa kuwa ana watoto saba.

Yamina alisema kuwa mahakama ya Shanzu haikuzingatia kwamba uchunguzi wa kesi hiyo bado unaendelea na kuachiliwa huru kwa mshukiwa huyo huenda kukatatiza uchunguzi huo.

Alidai kuwa huenda mshukiwa huyo akawatishia mashahidi wa kesi hiyo.

Wiki iliyopita, Hakimu Diana Mochache wa Mahakama ya Shanzu alitoa dhamana ya shilngi miliioni moja kwa mke wa Rogo na kisha kuisitisha kwa muda wa siku saba.

Saggar anahusishwa na mitandao ya kigaidi nchini Australia na Syria, pamoja na shambulizi la kigaidi katika Kituo cha polisi cha Central mjini Mombasa.