Benki kuu ya Kenya na Imperial zimepata pigo baada ya mahakama kuu kusimamisha kwa muda mpango wa kuwalipa wateja wa benki ya Imperial hadi kesi iliyowasilishwa na mfanyibiashara  Ashok Doshi itakapotamatika.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Hatua hii inajiri baada ya Doshi kuelekea mahakamani siku ya Jumanne, kuishtaki benki hizo mbili kwa kushindwa kumlipa shilingi bilioni moja anazodai benki ya Imperial baada ya kufungwa kwa benki hiyo.

Siku ya Jumatano, jaji wa mahakama kuu ya Mombasa, Patrick Otieno, aliagiza kusitishwa kwa mpango huo kwa wateja wote wa Imperial hadi kesi hiyo itakapo amuliwa.

Doshi anapinga mpango wa urasimu wa benki kuu wa kumlipa shilingi milioni moja kila mwezi.

Kesi hiyo itasikilizwa Mei 5, 2016.