Jaji mkuu nchini David Maraga katika hafla ya awali. [Photo/ the-star.co.ke]

Share news tips with us here at Hivisasa

Idara ya Mahakama nchini inapanga kujenga mahakama mbili mpya katika Kaunti ya Mombasa ili kupunguza mrundikano wa kesi.

Akizungumza katika jengo la Mahakama ya Mombasa siku ya Jumanne, Jaji mkuu nchini David Maraga alisema kuwa mahakama hizo zitajengwa katika eneo bunge la Likoni na Changamwe.

“Tutajenga mahakama mbili hivi karibuni ili tuweze kurahisisha kazi na kupunguza mrundikano wa kesi katika Mahakama ya Mombasa,” alisema Maraga.

Aidha, alisema wanapanga kuboresha na kurekebisha Mahakama ya Mombasa pamoja na ile ya Shanzu.

“Tutaifanyia marekebisho jengo la Mahakama ya Mombasa ili wafanyakazi waweze kuhudumu katika mazingira bora,” alisema Maraga.

Wakati huo huo, Maraga alisema kuwa wanamipango ya kumaliza kesi zote kwa haraka ili Wakenya waweze kupata haki zao kwa muda ufao.

“Tutaharakisha kusikiza kesi zote kwa haraka ili usawa na haki upatikane,” alisema Maraga.