Mahakama ya Mombasa imeagiza kutiwa mbaroni kwa mabwenyenye watatu wanaokabiliwa na madai ya kugushi vyeti vya umiliki wa nyumba ya mtu aliyefariki.

Share news tips with us here at Hivisasa

Paresh Shivji Jadva, Shivji Jadra Parbal na Victor Arara Were wanadaiwa kugushi vyeti vya umuliki wa nyumba ya mwendazake Premji Manji Pindolia, yenye thamani ya shilingi milioni 20.

Agizo hili linajiri baada ya afisi ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma kuwasilisha ombi hilo la kutiwa mbaroni kwa watatu hao.

Hakimu Edgar Kagoni alikubali ombi hilo siku ya Alhamisi na kuagiza kufikishwa kizimbani wakati wowote pindi watakapokamatwa.

Kesi hiyo itatajwa tena Agosti 28 mwaka huu, ambapo mabwenyenye hao watafunguliwa mashtaka.