Mahakama ya Mombasa imeagiza kutiwa mbaroni kwa waliohusika katika uchomaji wa meli iliyokuwa na dawa za kulevya pasi idhini ya mahakama.
Agizo hili limetolewa na Hakimu Julius Nang'ea aliyesema kuwa meli hiyo ilikuwa ushahidi muhimu katika kesi hiyo.
“Meli hiyo ilikuwa ushahidi muhimu kwa kesi hii. Sasa kesi imelemazwa kwa sababu ushahidi mkuu haupatikani,” alisema Nang'ea.
Nang'ea ameitaja hatua ya kuichoma meli hiyo kama ukiukaji wa katiba ya nchini na kuingilia uhuru wa idara ya mahakama.
Ikumbukwe kuwa Hakimu Nang'ea alikuwa amejiondoa kwenye kesi hiyo baada ya meli hiyo kukosekana kama ushahidi.
Meli hiyo kwa jina Baby Iris, ilizamishwa baharini mnamo Agosti mwaka 2015, baada ya kupatikana na heroini yenye thamani ya shilingi milioni 20.
Waziri wa usalama wa ndani Joseph Nkaissery alihudhuria ulipuaji wa meli hiyo baharini.