Mahakama kuu ya Mombasa imetoa agizo la kutiwa mbaroni kwa raia wa Marekani aliyehusishwa na mauaji eneo la Malindi.
Jacob Schmalzle anadaiwa kuhusika katika mauaji ya Jimmy Jagatram Baburam katika mkahawa wa Medina Palms Resort huko Watamu, mnamo Julai 26, mwaka jana.
Mahakama ilielezwa kuwa Schmalzle anadaiwa kushirikiana na Amina Shiraz kumuua muwewe, Baburam.
Jaji Asenatha Ongeri ametoa agizo hilo baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha ombi hilo mahakamani.
Hapo awali, kesi hiyo ilikuwa katika Mahakama ya Malindi lakini ikahamishwa hadi katika Mahakama kuu ya Mombasa.
Hii ni baada ya Jaji Said Chitembwe kujiondoa kwa kesi hiyo, baada ya mmoja wa karani kaika mahakama hiyo kudaiwa kupokea hongo, ili kusambaratisha kesi hiyo.