Mbunge wa Nyali Mohammed Ali katika hafla ya awali. [Picha/ the-star.co.ke]
Makahama kuu ya Mombasa imedinda kutupilia mbali kesi ya kupinga ushindi wa mbunge wa Nyali Mohamed Ali.Akitoa uamuzi huo siku ya Alhamisi, Hakimu Lydia Achode alisema kuwa hakuna sababu za kutosha za kutupilia mbali kesi hiyo.“Hakuna sababu mwafaka zilizotolewa za kufanya mahakama kutupilia mbali kesi hii,” alisema Achode.Achode aliongeza kuwa sharti kesi hiyo iendelee ili haki ya wapigakura ipatikane.“Kesi hii lazima iendelee kusikizwa ili pande zote mbili pamoja na wapiga kura wapate haki na uwazi,” alisema Achode.Uamuzi huu unajiri baada ya Mbunge Mohammed Ali kuwasilisha ombi la kutaka kutupiliwa mbali kwa kesi hiyo,kwa kusema kuwa haiambatani na kanuni za kesi za uchaguzi.Aidha, Ali alisema kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa haki na uwazi kufuatia hatua ya wakaazi wa Nyali kutekeleza haki yao kikatiba.Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani na mpiga kura Daniel Ongong’a Abwao ambaye alidai kuwa uchaguzi huo haukuwa wa haki na uwazi.Abwao ameitaka mahakama kufutilia mbali ushindi huo ili uchaguzi mpya kufanyika.Kesi hiyo itasikizwa Januari 8, 2018.