Jengo la Mahakama ya Mombasa.[Photo/ the-star.co.ke]

Share news tips with us here at Hivisasa

Mahakama Kuu ya Mombasa imedinda kuhamisha masanduku pamoja na vifaa vya kupigia kura vilivyotumika kwenye uchaguzi wa Agosti 8 katika eneo bunge la Changamwe.Mahakama hiyo pia imedinda kutia kufuli jumba ambalo masanduku hayo pamoja na vifaa vya kura vinahifadhiwa.Hii ni baada ya Abdi Daib ambaye aliwasilisha kesi mahakamani kupinga ushindi wa mbunge Omar Mwinyi kuwasilisha ombi hilo mbele ya Jaji Njoki Mwangi.Wakili Gikandi Ngubuin, anayemwakilisha Abdi, aliitaka mahakama kuhamisha masanduku hayo hadi katika jengo la Mahakama ya Mombosa ili yahifadhiwe huko.Aidha, ameitaka mahakama kuu kuhakikisha kuwa pande zote zinaweka vibanio kwenye masanduku hayo, ili yasiweze kufunguliwa bila ya amri ya mahakama.Wakati huo huo, Gikandi ameitaka mahakama kufunga kwa kufuli jumba ambalo masanduku hayo yanahifadhi kama njia ya kuyaepusha kufunguliwa.Jaji Njoki amedinda kuhamisha masanduku hayo pamoja na kufunga jumba ambalo masanduku hayo yanahifadhiwa kwa kuwa jumba hilo linatumika kuhifadhi masanduku ya wagombea tofauti.Mahakama imeagiza pande zote kuweka vibanio vyao kwenye masanduku hayo.Kesi hiyo itasikilizwa Oktoba 23, 2017 huku zaidi ya mashahidi 50 wakitarajiwa kutoa ushahidi wao.