Mbunge wa Likoni Mishi Mboko akiwa katika Mahakama ya Mombasa hapo awali. [Picha/ nation.co.ke]

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mahakama kuu ya Mombasa imedinda kutupilia mbali kesi ya kupinga ushindi wa Mbunge wa Likoni Mishi Mboko.Ombi hilo liliwasilishwa mahakamani na Mboko, kwa madai kuwa kesi hiyo haikuwa imetimiza vigezo vya sheria za uchaguzi. Akitoa uamuzi huo siku ya Jumatano, Hakimu Erick Ogola alisema kuwa hakuna sababu kuu zilizowasilishwa mbele ya mahakama ambazo zingesababisha kesi hiyo kufutiliwa mbali.“Hakuna sababu kuu za kunifanya nitupilie mbali kesi hii. Sharti kesi hii iendelee kwa manufaa ya wapigakura wa Likoni,” alisema Ogola.Jaji Ogola alisema kesi hiyo imetimiza vigezo vyote vya kesi za uchaguzi kwa mujibu wa katiba.“Vigezo na kanuni zote za kesi za uchaguzi zimezingatiwa kwenye kesi hii, kinyume na inavyodaiwa na Mishi Mboko,” alisema Ogola.Aidha, Jaji Ogola ameagiza masanduku na makaratasi ya uchaguzi wa ubunge Likoni yaliyotumika katika uchaguzi wa Agosti 8, kuhifadhiwa chini ya ulinzi mkali ikizingatiwa ni miongoni mwa ushahidi katika kesi hiyo.Wiki chache zilizopita, Mboko kupitia wakili wake Paul Butti aliwasilisha ombi kutaka kesi hiyo itupiliwe mbali kwa madai kuwa ilikiuka sheria za kesi za uchaguzi.Kesi hiyo ya kupinga ushindi wa Mboko iliwasilishwa mahakamani na aliyekuwa mbunge wa Likoni Masoud Mwahima.