Jengo la Mahakama ya Mombasa. [Picha/ barakafm.org]

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mahakama kuu ya Mombasa imetakiwa kutupilia mbali kesi ya mzozo kati ya kituo cha redio cha Baraka FM na baadhi ya viongozi wa dini jijini Mombasa kuhusiana na vipindi vinavyoendeshwa na kituo hicho.Kesi hiyo iliwasilishwa na baadhi ya wahubiri wakiongozwa na Jeremia Mugondson, waliodai kuwa Baraka FM imekiuka maadili ya dini ya Kikirsto katika vipindi vyao, ikizingatiwa kituo hicho kilianzishwa chini ya kanuni za dini hiyo.Wakili anayewakilisha kituo hicho Kennedy Ngaira, amesema kuwa mahakama kuu haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, na kuwataka wahubiri hao kuwasilisha malalamishi yao kwa halmashauri kuu ya kudhibiti vyombo ya habari nchini.Kwa upade wake, Leonard Shimaka, wakili anayesimamia wahubiri hao, amesema kituo hicho hakizingatii mafunzo ya dini katika vipindi vyao, licha ya kuwa kilifunguliwa chini ya muungano wa dini hiyo.Aidha, amesema kuwa wahubiri hao wametengwa katika uendeshaji wa kituo hicho katika ngazi za wakurugenzi wakuu.Jaji Erick Ogola atatoa uamuzi wake tarehe Disemba 19 mwaka huu.