Tume ya kupambana na ufisadi nchini imepewa ruhusa kumchunguza aliyekuwa mbunge wa Mswambeni Omari Zonga kuhusu unyakuzi wa ardhi inayomkabili.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kipande hicho cha ardhi cha hekari 22 kilichoko kaunti ya kwale wakati mmoja kilikuwa kinamilikiwa na mtoto wa mfalme Sadrudin Aga khan.

Jaji Edward Muriithi alisema mahakama haingeweza kumpa Zonga, Raia Mkungu, Said Kabangi na Hiimi Ahmed amri ya kupewa umiliki wa kipande hicho cha ardhi chenye mzozo hadi uchunguzi utakapokamilika.

Muriithi alikataa maombi ya Zonga ya kutaka tume ya EACC kutoingilia swala la ardhi yao ambayo waliirithi kutoka kwa wazee wao.

Zonga na wenzake watatu wanasema kuwa kipande hicho cha ardhi kilikuwa cha babu yao Mwachimwindi Diya, ambaye aliondolewa kwenye sehemu hio na serikali ya waingereza kabla ya uhuru.