Mahakama moja jijini Mombasa imetupilia mbali ombi la kumtaka mwanaharakati Mgandi Kalinga kutoa namba yake ya siri ya simu kwa maafisa wa usalama ili kukamilisha uchunguzi wao dhidi ya kesi ya utumizi mbaya wa vyombo vya mawasiliano.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwanaharakati huyo anakabiliwa na kesi ya kutumia mtandao wa WhatsApp kumtusi Seneta Mteule Emma Mbura.

Akitoa uamuzi wake siku ya Alhamisi, Hakimu Nicholas Njangi alisema kuwa ombi lililowasishwa na upande wa mashtaka halina msingi wowote ikizingatiwa uchunguzi ulifanywa kabla ya mwanaharakati huyo kufunguliwa mashtaka.

Hatua hii inajiri baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha ombi hilo la kumtaka Kalinga toa nambari hiyo kwa polisi kwa uchunguzi zaidi.

Itakumbukwa Jaji Mumbi Ngugi alitupilia mbali kifungu nambari 29 katika Sheria ya Habari na Mawasiliano Nambari 3 ya 1998 ambacho hutumika kuwafungulia mashtaka wanaotumia vyombo vya mawasiliano kwa njia isiyofaa.

Jaji Mumbi alisema kifungu hicho cha kutumia vibaya kifaa cha mawasiliano kinakiuka katiba.

Kifungu hicho hupendekeza faini ya Sh50,000 au kifungo cha miezi mitatu jela, au adhabu zote mbili, kwa mtu anayepatikana na hatia.