Mshukiwa wa ugaidi, Idi Lukoko Oswundwa, ameachiliwa huru na Mahakama ya Mombasa.
Hii ni baada ya kukosekana ushahidi wa kutosha wa kumfungulia mashtaka ya ugaidi.
Upande wa mashtaka uliwasilisha ombi la kutaka mahakama kumuachilia huru Lukoko, kwa kusema kuwa kesi hiyo haiwezi kuendelea bila ushahidi wa kutosha.
Hakimu Daglous Ogoti alikubali ombi hilo siku ya Ijumaa na kumuachiliwa huru.
Lukoko alitiwa mbaroni juma lililopita katika Kaunti ya Kwale alipohusishwa na visa vya ugaidi, baada ya kukosa kuwasilisha kitambulisho cha kitaifa.
Hatua hii ilimfanya kuzuiliwa rumande kwa siku nane huku akisubiri uchunguzi kukamilika.