Juhudi za gavana wa Garissa, Nathif Jama kusimamisha kesi dhidi yake iliambulia patupu hapo Jumatano pale mahakama ilipo kataa ombi lake ya kesi hiyo kusimamishwa.
Mahakama ya juu ilipinga ombi lake lakini ikatoa amri ya kumruhusu asikamatwe baada ya siku ishirini na moja.
Hakimu Weldon Korir katika hukumu yake alisema kuwa hakuona ushahidi yoyote ambayo inaunga mkono Jama anayedai kuwa mkurugenzi wa mashtaka ya umma, DPP pamoja na tume ya maadili na kupambana na ufisadi ilivyo tumia mamlaka yao vibaya, EACC.
Korir alisema kwamba madai ya Jama kuwa viongozi wenye usemi katika serikali wanapinga uongozi wake hayana msingi huku akisisitiza kuwa ni korti tu ndio itadhihirisha ukweli.
Jama alijipata matatani pale aliporuhusu kaunti ya Garissa kuweka mkataba wa kutumia magari ya wagonjwa (ambulance) ambayo yalilipiwa sh650,000 kila mwezi kutoka kwa shirika la msalaba mwekundu.