Mahakama Kuu ya Mombasa imesimamishha kwa muda hatua ya kuwafungulia wawakilishi wadi wawili kutoka Kaunti ya Lamu mashtaka ya uchochezi.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwakilishi wadi mteule Monica Kirunyu na mwenzake wa Wadi ya Bahari Antony Maina wanakabiliwa na madai ya kuwachochea wakaazi wa maeneo hayo.

Wawili hao wamewasilisha ombi la kusimamisha kufunguliwa mashtaka hayo mbele ya Mahakama ya Mombasa.

Siku ya Jumanne, Jaji Dora Chepkonywi alisimamisha kesi inayowakabili wawili hao, hadi kesi iliyoko mbele yake kukamilika.

“Nimesimamisha kuendelea kwa kesi hii katika mahakama ya chini, mpaka ombi hili lililoko mbele yangu kukamilika,” alisema jaji Chepkonywi.

Agizo la kutiwa mbaroni kwa wawili hao lilitolewa mnamo Oktoba 12, mwaka huu, baada ya kukosa kufika kizimbani kusomewa mashtaka.

Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani na Tume ya uwiano na utengamano nchini NCIC, na itaendelea siku ya Jumatano.