Mahakama kuu jijini Mombasa imesitisha ubomozi wa nyumba za makaazi katika eneo la Kwa Punda, Changamwe, hadi pale kesi hiyo itakapokamilika.
Akitoa uamuzi huo siku ya Alhamisi, Jaji Omolo alisema kuwa hakuna ubomozi utakaoendelea hadi kesi hiyo itakapo amuliwa ili kubaini wahusika halali.
Kesi hiyo ya mzozo wa ardhi inahusisha zaidi ya familia 300 ambazo zinadai kufurushwa na wamiliki wa kampuni ya Garisa Matresses Ltd mwaka jana.
Wakaazi wa eneo hilo wameonyesha furaha yao na kupongeza uamuzi wa mahakama kwa kusema haki imeanza kupaatikana kwa wanyonge.
Wakiongozwa na Samuel Kamau, wakaazi hao walisema kila wanapokuwa na matatizo ya ardhi watakimbilia kotini ili kutafuta haki.
“Tuna furaha sana kwa kusimamishwa kwa ubomozi wowote katika shamba hilo la ekari 75,” alisema Kamau.